Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Halmashauri ya Mji wa Geita kuanza kutoza faini ya Laki 2 mpaka Milioni 1 kwa uchafuzi wa mazingira

Katika kuimarisha hali ya usafi wa mazingira ndani ya Halmashauri ya Mji wa Geita Halmashauri hiyo imetangaza kutoza faini kuanzia kiasi cha shilingi laki mbilii hadi milioni moja kwa wananchi watakaobainika kuchafua mazingira ikiwa ni hatua ya kukomesha tabia ya kutupa taka hovyo hali ambayo imekuwa ikisababisha mji huo kuonekanaa mchafu kila kukicha.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita Yefred Myenzi wakati akizungumza na Jambo Fm ambapo amesema ili kuufanya mji wa Geita kuwa miongoni mwa Miji safi hapa nchini ni jukumu la kila mkazi kutunza mazingira na katika kulitekeleza hilo halmashauri italazimika kutoza kiasi hicho cha pesa kwa wale wote watakaohusika na uchafunzi wa mzingira.
Aidha Myenzi amesema utaratibu wa awali wa ukusanyaji wa taka ndani ya Halmashauri ya Mji wa Geita haukuwa sawa hali iliyopelekea mji huo kuwa mchafu hivyo kwa sasa halmashauri hiyo imelazimika kumtafuta mkandarasi atakaye husika kukusanya taka katika maeneo yote ya Mji wa Geita ili kuufanya mji kuwa safi wakati wote.

Mmoja wa wakazi wa mji wa Geita Sagal Mganga amesema baadhi ya wakazi wa mji huo wamekuwa wakichafua mazingira kwa kutupa taka hovyo hivyo ili adhabu hiyo iweze kuendana na uhalisia ni vyema halimashauri ikahakikisha kwanza inaondoa uchafu wote katika maneo ya mjini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *