Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Vijiji 17 mkoani Geita vinakwenda kunufaika na mradi wa ujenzi wa minara ya mawasiliano – Waziri Nape

Serikali imetoa zaidi ya shilingi Bilioni 200 kwa lengo la kujenga minara ya mawasiliano vijijini hapa nchini ili kuboresha huduma ya mawasiliano katika maeneo mbalimbali ya vijiji na kuondoa kero ya ukosefu wa huduma sitahiki za mawasiliano zinazowakabili wakazi wengi wa maeneo ya vijijini.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nauye wakati akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Luhuha Kata ya Nyakagomba Wilayani Geita Mkoani Geita baada ya kutembelea ujenzi wa mnara unaojengwa katika kijiji hicho ambapo amesema serikali inatarajia kujenga minara zaidi ya 700 ambapo mkoa wa geita tayari umetengewa kiasi cha shilingi bilioni 2.2 kwa ajili ya ujenzi wa minara 17 katika maeneo mbalimbali ya vijiji vya wilaya hiyo.

Awali akizungumza katika uzinduzi wa mnara huo Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela ameipongeza serikali kwa kutoa pesa za ujenzi wa minara hiyo 17 kwani upatikanaji wa huduma za mawasiliano vijijini utarahisisha shughuli za uchimbaji wa madini kwa kutumia mitambo ya kisasa pamoja na kukuza uchumi wa wakazi wa mkoa huo.

Nao baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Luhusa wamesema kabla ya ujezi wa mnara huo wamekuwa wamekuwa wakikosa huduma za kimtandao huku wakilalamikia changamoto ya kuuziwa vocha kwa gharama kubwa kwani vocha ya shilingi 1000 wanauziwa 1200 na vocha ya shilingi 500 wanauziwa kwa shilingi 600.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *