Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Rais Samia mgeni rasmi maadhimisho ya kupinga dawa za kulevya Mwanza

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan,anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kupinga dawa za kulevya ambayo kitaifa yanatarajia kufanyika katika jiji la Mwanza.


Akizungumza na waandishi wa habari hii leo mkuu wa mkoa wa Mwanza Said Mtanda amesema maadhimisho hayo yanatarajia kuanza hii leo tarehe 28/06/2024 katika viwanja vya Nyamagana na yatahitimishwa tarehe 30/062024 katika viwanja hivyo ambapo mgeni rasmi atakua Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania dk. Samia Suluhu Hasani.


Kufuatia maadhimisho hayo Mtanda amewaalika wananchi wa mkoa wa Mwanza na maeneo mengine kufika katika uwanja wa Nyamagana kwani kutakua na shughuli mbalimbali zinazoendela ikiwemo kongamano maalumu ambalo litakua linatoa elimu juu ya athari za madawa ya kulevya.


Maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kupambana na dawa za kulevya kwa mwaka huu itakua inaongozwa na kaulimbiu isemeyo “ Wekeza kwenye kinga na tiba dhidi ya dawa za kulevya”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *