Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

DC Geita Apiga Marufuku Wananchi Kutozwa Fedha Kuvuka Daraja

Na Costantine James,Geita

Mkuu wa wilaya ya Geita Hashim Komba amepiga marufuku wananchi kutozwa fedha wakati wa kuvuka daraja la muda kutoka Kijiji cha Nyakabale kuelekea Nyamatagata katika Kata ya Mgusu wilayani humo Mkoani Geita hali ambayo imekuwa ikileta changamoto kubwa kwa wananchi wa eneo hilo na kusababisha shughuli za kiuchumi kukwama.

DC Komba ametoa agizo hilo leo (Juni 21, 2024) wakati wa ziara yake ya kukagua miradi na kusikiliza kero za wananchi katika kata hiyo mara baada ya kufika katika daraja hilo na kukuta ujenzi unasuasua huku wananchi wakitozwa fedha kuvuka daraja mbadala lililojengwa katika eneo hilo licha ya serikali kutoa fedha za ujenzi wa daraja la muda ili wananchi waweze kupita wakati ujenzi wa daraja la kudumu ukiendelea.

Awali akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo Mwakilishi wa Meneja wa TARURA wilaya ya Geita Bw. Simon Buganga amesema ujenzi wa daraja hilo umeanza Februari 29,2024 ukitarajiwa kukamilika Juni,2024 kwa gaharama ya milioni 400 huku akisema kabla ya kuanza ujenzi wa daraja hilo wananchi walikua wanatozwa na mtu binafisi aliyejenga daraja la muda lakini baada ya kuanza ujenzi wamlipa fidia na kuondoka.

Mkandarasi anayetekeleza ujenzi wa daraja hilo kutoka kampuni ya YUNICON ya jijini Mwanza Thurston Mgeni amesema sababu kubwa zilizopelekea daraja hilo kushindwa kukamilika kwa wakati ni mvua kubwa zilizonyesha marchi, 2024 nakusababisha ujenzi kukwama huku akiomba kuongezewa siku 60 nje ya mda wa mwanzo ili kumaliza ujenzi wa daraja hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *