Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Mradi Wa Maji Watelekezwa Baada ya Kukamilika

Na Costantine James,Geita

Mkuu wa wilaya ya Geita Hashim Komba hii leo Juni 20,2024 amelazimika kusitisha Mkutano wa hadhara uliokuwa na lengo la kusikiliza kero za wananchi katika mtaa wa Ikulwa kata ya Ihanamilo Halmashauri ya Mji wa Geita na kwenda kujionea   mradi wa maji ulionza kutekelezwa tangu mwaka 2022 kwa lengo la hudumia kata hiyo ambapo kutokamilika kwake kusababisha wananchi kuendelea kukosa huduma ya maji licha ya mradi uwepo wa mradi.

Hatua hiyo imekuja baada ya Diwani wa kata ya Ihanamilo Joseph Lugayila kulalamikia changamoto ya ukosefu wa huduma ya maji katika kata hiyo licha ya mradi kukamilika katika kipindi ambacho Mamlaka ya Maji na Usafi wa mazingira Halmashauri ya Mji wa Geita (GEUWASA) na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) zikitupiana mpira wa nani mmiliki wa mradi huo.

Baada ya kufika katika mradi huo Dc Komba ameshuhudia utelekezwaji wa radi husika licha ya kukamilika na kutoa maelekezo ya serikali (GEUWASA) na (RUWASA) akiwataka kufika mara moja katika mradi huo kufanya suluhu ya haraka ili wananchi waanze kunufaika na uwepo wake.

Akielezea historia ya mradi huo mwenyekiti wa mtaa wa Wigembya Bw. Sebastian Kitobelo amesema ujenzi wa mradi huo ulianza mwaka 2022 na ulipokamilika ulianza kufanyiwa majaribio na kutoa maji kwa njia ya umeme wa sola na baadae kuingizwa umeme,lakini baada ya hapo wahusika hawakuonekana tena na baadae kupewa taarifa ya kwamba mradi huo umehamishwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *