Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Wenye Viwanda Waibariki Bajeti ya 2024-2025

Shirikisho la Wenye Viwanda nchini (CTI), limepongeza bajeti kuu ya serikali kwa kuweka mambo muhimu ambayo yatachochea ukuaji wa viwanda nchini wakati wa utekelezwaji wa bajeti hiyo.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa shirikisho hilo, Leodegar Tenga, wakati akizungumza na waandishi wa habari na kubainisha kwamba serikali imekuwa sikivu kwa wenye viwanda na kila wanapokuwa na jambo wamekuwa wakifunguliwa milango ya majadiliano na kwamba hakuna jambo la wenye viwanda ambalo linakwama.

Amesema wenye viwanda wamefurahia bajeti ya serikali kwa kuzingatia uendelezaji wa miradi ya kimkakati kama reli ya kisasa SGR ambayo amesema itasiadia kwa kiwango kikubwa kukuza viwanda vya ndani kuzalisha kwa wingi bidhaa.

“Nchi ambayo iko makini inaendeleza miradi mikubwa kama ya ujenzi wa reli, barabara, miradi ya maji kama kuendeleza miradi ya kimkakati barabara maji, bandari kwasababu huwezi kuendeleza viwanda kama huna umeme au unamatatizo ya usafirishaji,mfano bei ya mfuko wa saruji hapa Dar inaweza kuwa shilingi 16, 00017 au 17,000 lakini bei ya kuubeba mpaka Mwanza ni kati ya shilingi 10,000 hadi 12,000 kwa hiyo mtu ananunua mfuko wa saruji hapa kwa Shilingi 16, 000 lakini mpaka kuufikisha Mwanza unauzwa shilingi 28,000,” amesema Bw.Tenga

Bw.Tenga pia amesema bajeti ya mwaka huu inakusudia kuhamasisha mapato ya ndani zaidi ikilinganishwa na bajeti ya 2023/24 na kubainisha kwamba jambo muhimu katika bajeti ya mwaka huu ni Serikali kufanya mageuzi mbalimbali ya muundo wa kodi, ada, tozo na marekebisho ya sheria na kanuni ili kuboresha mazingira ya biashara na marekebisho ambayo yamependekezwa kuhusiana na sekta ya viwanda ni katika ongezeko la thamani VAT, ushuru wa bidhaa, ada na tozo za wakala pamoja na ushuru wa forodha.

Ameelezea baadhi ya hatua chanya kuwa ni pamoja na kuanzishwa kwa tozo ya maendeleo ya viwanda kwa bidhaa zinazotoka nje yenye lengo la kulinda viwanda vya ndani, kuchochea uwekezaji na kuongeza mauzo ya nje; kupunguza ada na tozo zinazotolewa na vyombo vya udhibiti ili kupunguza gharama za uzalishaji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *