![](https://jambofm.co.tz/wp-content/uploads/2023/06/NYONII.png)
Klabu ya Namungo FC imetangaza kumsajili aliyekuwa mlinzi wa Simba SC, Erasto Edward Nyoni, ikiwa ni siku moja tu baada ya kuachwa msimbazi.
Taarifa ya klabu hiyo imesema:”Tunayofuraha kuwataarifu kuwa Erasto Edward Nyoni amejiunga kuitumikia Timu yetu ya Namungo Fc akitokea Simba Sc.
“Karibu kwenye Familia ya Wauwaji wa Kusini Erasto Edward Nyoni”