Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Uingereza Walalamikia Bei ya Mafuta Kutopungua Tangu Aprili

Umoja wa Kundi la Madereva wa magari nchini Uingereza (RAC) hivi sasa wanalalama wakisema hakuna sababu nzuri kwa nini bei za mafuta hazijapunguzwa ikiwa gharama za jumla za ununuzi wa nishati hiyo zimeshuka tangu mwisho wa Aprili na kutoa wito kwa mamlaka husika kuchukua hatua kushughulikia hilo.

Aidha Wauzaji wa reja reja wa mafuta wameshutumiwa kwa kutumia kigezo cha wa uchaguzi mkuu kuwa sababu ya bei ya petroli na dizeli kuzidi kuongezeka unaotarajiwa kufanyika tarehe 4 Julai 2024.

Umoja huo unasema gharama imekuwa juu zaidi kuliko inavyotarajiwa kwa kuwa gharama za jumla zimeshuka tangu mwisho wa Aprili na Bei ya wastani ya lita moja ya petroli nchini Uingereza kwa sasa inalezwa kuwa ghali Zaidi kuliko ilivyotarajiwa na kuelezwa kwamba bei ya nishati hiyo iko juu Zaidi kuliko ilivyo katika Mataifa ya Ireland Kaskazini ambako kwa mataifa ya Ulaya ni taifa pekee ambalo bei ya mafuta iko chini zaidi.

Wamelalama Wakisema Takwimu zinaonyesha wazi kuwa bei za mafuta hazijashuka sanjari na kupunguzwa kwa bei ya jumla, kwa hivyo madereva kote Uingereza – isipokuwa wale wa Ireland Kaskazini ambapo bei nzuri hutozwa – kwa mara nyingine tena wanapoteza pauni kadhaa kila wakati wanapojaza mafuta.

Wameongeza kwamba tunaamini hakuna sababu nzuri kwa wauzaji wa rejareja nchini Uingereza kutopunguza bei zao kwenye pampu mbali zaidi,tunaweza kufikiria tu kwamba wanatumai hakuna mtu atakayegundua kutokana na kuvurugwa na uchaguzi mkuu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *