Shinyanga: Hoja 31 za CAG zakosa majibu

Serikali Mkoani Shinyanga, Imebainisha Sababu Tano Ambazo Zinasababisha Hoja Za Mdhibiti Na Mkaguzi Mkuu Wa Hesabu Za Serikali (CAG) Kukosa Majibu Katika Halmashauri Za Msalala, Kutumia Fedha Pasipo Kupata Kibali Cha Matumizi Kutoka Kamati Ya Fedha Ya Halmashauri Hiyo.

Halmashauri Hiyo Ilikuwa Na Hoja 59, Kati Ya Hizo Hoja 28 Zimefungwa Kwa Kutafutiwa Majibu Na Hoja 31 Bado Zinaendelea Kushughulikiwa Hivyo Bila Kupata Vielelezo Vinavyohitaji, Hoja Hizo Zitaendelea Kukosa Majibu Kila Mwaka Wa Fedha.

Hayo Yamebainishwa Na Mkuu Wa Mkoa Wa Shinyanga Christina Mndeme Kwenye Mkutano Maalum Wa Baraza La Madiwani La Halmashauri Hiyo kwa lengo La Kupitia Na Kujadili Taarifa CAG ambapo Amesema, Moja Ya Sababu Inayosababisha Kuwepo Kwa Hoja Hizo Ni Ukosefu Wa Hati Miliki Kwa Maeneo Yaliyotumika Kujenga Majengo Ya Halmashauri.

Mndeme Ameongeza Kuwa Sababu Ya Pili Ni Makusanyo Ya Mapato Ya Ndani Kiasi Cha Sh. Milioni 214.5 Yaliyokusanywa Kwa Mashine Za Posi Hayakupelekwa Benki Kwa Wakati Na Kusababisha Kuibuka Kwa Hofu Ya Fedha Hizo Na Kushindwa Kuwa Na Taarifa Sahihi Kwanini Hazikupelekwa Benki.

Comments are closed.