Anguko kama la ANC Lamkumba Waziri Mkuu wa India

Matokeo ya uchaguzi nchini India yemeonesha kuwa chama cha BJP cha Waziri Mkuu Narendra Modi kimepoteza wingi wa viti bungeni ili kukiwezesha kubaki pekee hili likiwa sawa na kilichotokea kwa chama cha ANC nchini Afrika Kusini.

Licha ya Waziri Mkuu wa India Narendra Modi kushinda muhula wake wa tatu mfululizo, lakini chama chake cha BJP hakikupata wingi wa wawakilishi bungeni kama kilivyotarajia ili kukiwezesha chama hicho kuiongoza India, na sasa BJP kinahitaji kutafuta washirika kutoka vyama vingine vya kisiasa ili kuunda serikali ya mseto.

Chama cha Waziri Mkuu Narendra Modi, kimepoteza wingi wa viti bungeni kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 10 katika Uchaguzi Mkuu wa India na miongoni mwa nchi zilizompongeza Narendra Modi ni pamoja na China ambyo Msemaji wa Wizara yake ya Mambo ya Nje Mao Ning, amesema nchi yake iko tayari kushirikiana na jirani yake huyo.

Matokeo yaliyotolewa rasmi  jumatano na Tume ya Uchaguzi ya India yalionyesha kuwa vyama vinavyomuunga mkono Waziri Mkuu Narendra Modi vimepata viti vingi kuliko chama cha National Democratic Alliance (NDA) katika uchaguzi huo mkuu uliomalizika baada ya kufanyika kwa muda wa wiki sita. 

Wagombea wa ubunge wa chama hicho cha NDA wengi wao waliangushwa hali iliyomsababishia Modi mashangao kutokana na Waziri Mkuu huyo wa India aliamini kwamba chama hicho kingeshinda kwa kishindo kwa kupata viti zaidi ya 400 lakini haikuwa hivyo.

Muungano wa vyama vinavyokiunga mkono chama hicho cha NDA ambavyo kwa pamoja vinaunda chama cha BJP ulishinda katika maeneo bunge 294 pekee,chama kinachotawala nchini India cha BJP kikiwa kimepata jumla ya viti 240 tu, ikilinganishwa na viti 303 kilivyovipata katika uchaguzi uliopita wa mwaka 2019.

Hivi sasa chama hicho cha BJP kinahitaji kutafuta uungwaji mkono na vyama vingine vya siasa ili kuweza kufikisha viti 272 au zaidi katika bunge lenye jumla ya viti 543 ili kiweze kuwa madarakani.

Wakati huo huo, wafuasi wa chama kikuu cha upinzani cha Indian National Congress kinachoongozwa na Rahul Gandhi, walionekana kuwa na furaha licha ya chama chao kushindwa katika uchaguzi huo mkuu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *