Idris Sultan alipokuwa akihojiwa moja kati ya maswali aliyoulizwa ni kuwa ni kweli Tasnia ya burudani nchini Tanzania imepitwa na ya Nchini Kenya kwakua Kenya wana kazi nyingi kimataifa kuliko Tanzania, jibu lake likawa ni ‘Kind off’.
Mtangazaji wa ‘The Chanzo’ alimuuliza Idris Sultan kwanini Kenya ina filamu nyingi kwenye Mtandao wa Netflix na channel ya ‘Showmax’ kwa upande wa Afrika Mashariki kwani wao wanatuzidi nini?
Idris Sultan alianza kwa kusema ‘Hapo ndio sehemu ambao unaniuliza swali ambalo lina jibu haya kuliko yote’
“Hawajatuzidi Leo Kwa bahati mbaya, wametuzidi zamani kidogo na hiyo zamani ndio ime-determine Leo yao na ilikua ni lugha (kiingereza). Na sio kwenye kutuzidi labda kwenye kuongea, bali wamekitumia kwenye kazi zao za kisanaa.
” Na Kenya hawaongei kiingereza tu au kiswahili tu, bali wanachanganya kiswahili na Kiingereza, hii inawasaida kua na mfanano na Mataifa mengine,Sasa unapoingia kwenye majukwaa ya kimataifa kama yale (Netflix na Showmax) ukija kutengeza maudhui, unataka uweke maudhui ambayo watu wengi katika mataifa tofauti wanaweza kuyaelewa na hapo ndipo lugha inaposaidia.
” Kwahiyo wao ‘Kenya’ tuseme tu walituwahi, lakini kwasasa hivi ukisema utuweke kwenye mzani mmoja na uangalie ni wapi wametuzidi kwenye Sanaa Kwa ujumla, kuanza ujuzi, vipaji na ubunifu ni wazi sisi tuko juu yao pakubwa sana kwenye sanaa kwa ujumla wake na sio muziki wala filamu tu peke yake”