Baraza la Seneti la Marekani Laidhinisha Muswada wa Misaada

Baraza la Seneti la Marekani limeidhinisha,kifurushi cha msaada wa mabilioni ya dola kwa Ukraine, Israel na Taiwan.

Katika jumla ya msaada huo wa dola bilioni 95, kiasi dola bilioni 61 zimetengwa kwa ajili ya jeshi la Ukraine ambalo linahitaji mno silaha na wanajeshi wapya.

Pia umeafiki kutoa dola bilioni 26 za msaada kutokana na vita vya Israel na dola bilioni 8 ili kukabiliana na ushawishi unaoongezeka wa China huko Taiwan na katika kanda ya Indo-Pacific.

Baraza la Seneti la Marekani pia limeidhinisha fedha za msaada wa kibinadamu unaohitajika kwa Gaza, Sudan na Haiti na pia umejumuisha pia uwezekano wa kuupiga marufuku mtandao wa kijamii wa TikTok nchini Marekani, ikiwa wamiliki wa China hawatouza hisa zao ndani ya kipindi cha mwaka mmoja.

Kinachosubiriwa hivi sasa ni Rais Joe Biden kukamilisha mchakato huo kwa kutia saini na katika Kipindi hiki ambacho ameapa kuwa vifaa zaidi vitawasilishwa haraka kwenye eneo la vita huko Ukraine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *