Mkuu wa ujumbe wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji nchini Djibouti Tanja Pacifico, ameliambia shirika moja la habari kwamba miili 21 imepatikana, huku watu 23 wakiwa bado hawajapatikana na wengine 33 wakinusurika kufuatia ajali ya boti ilivyotokea nchini Djibouti.
Hii ni ajali ya pili mbaya ya baharini ndani ya wiki mbili kutoka kwenye taifa hilo la Pembe ya Afrika, ambalo liko kwenye ile inayoitwa Njia ya Uhamiaji ya Mashariki kutoka Afrika hadi Mashariki ya Kati.
Meli nyingine iliyokuwa imebeba wahamiaji wengi wa Ethiopia ilizama katika eneo hilo hilo Aprili 8, na kupoteza maisha ya watu kadhaa.
Balozi wa Ethiopia nchini Djibouti, Berhanu Tsegaye,kupitia mtandao wa X amesema kwamba boti hiyo ilikuwa imebeba wahamiaji wa Ethiopia kutoka Yemen kabla ya kuzama Jumatatu usiku karibu na Godoria kaskazini Mashariki mwa Djibouti.