Barbara Gonzalez anatajwa kurejea Simba SC

Tetesi zilizopo ni kuwa Barbara Gonzalez, anatarajiwa kuchukua nafasi ya Salim Muhene “Try Again” baada ya kukubali kukaa pembeni hiyo yote ikisababishwa na timu kufanya vibaya katika mashindano mbalimbali iliyokuwa ikishiriki.

Desemba 10,2022 CEO Barbara aliandika barua ya kujiuzulu wadhifa wake kama Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba SC ambapo alieleza nia yake ya kuachia nafasi hiyo kuanzia Januari mwaka 2023

Simba Sc iliyokuwa chini yake ilipata mafanikio mafanikio makubwa ndani na nje ya uwanja, ikiwemo kutwaa mataji, kuvutia wafadhili na kuanza kuheshimika kama mojawapo ya vilabu vikubwa vya soka Afrika.

Endapo atarejea katika klabu hiyo atakuwa na kibarua kikubwa cha kuirejesha katika ubora wake baada ya kupoteza makali na kung’olewa katika michuano mbalimbali iliyokuwa ikishiriki ambayo ni pamoja na michuano ya klabu bingwa Afrika iliyoondolewa katika hatua ya makundi na Al Ahly,Michuano ya Kombe la Shirikisho Tanzania baada ya kufungwa na Mashujaa FC pamoja na kutokuwa na mwenendo mzuri katika ligi kuu Tanzania bara.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *