Young Killer awakumbuka wafungwa

Staa wa muziki kutoka Bongo anayewakilisha kipande cha Rock City (Mwanza) Youngkiller, akiongozana na mama yake mzazi pamoja na mpenzi wake wametembelea Gereza Kuu Butimba – Mwanza kutoa misaada ikiwemo vinjwaji, Dawa za meno, Miswaki na mafuta ya kupak wa wafungwa wa gereza hilo.

“Nmefurahi sana leo kufika Gereza Kuu Butimba – Mwanza na kukutana na ndugu zetu waliopata chagamoto za kuwapelekea kuwa gelezani. Ninamshukuru sana mwenyezi Mungu, kunipa hii nafasi ya kuwatembelea ndugu zetu, na pia nachukua nafasi hii kumshukuru Mkuu wa Gereza Kuu Butimba- Mwanza kutupokea vizuri na kuunga mkono nia yetu hii njema tuliyokuwa nayo,” ameandika msanii huyo kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Akaongeza “Pia nichukue nafasi hii kuomba radhi kwa atakayoona tofauti ya post hii, sio utaritibu wangu kuonesha vitu kama hivi Kwani siku zote hufanya kimya kimya, lakini kuweka hii Ni kuleta motishaa kwa wengine kuwajali pia hawa kwani nao pia wanauhitaji.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *