Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Watu milioni 55 wanakabiliwa na njaa Afrika

Takriban watu milioni 55 wanakabiliwa na kitisho cha njaa katika kanda ya Afrika Magharibi na Kati kutokana na kupanda kwa bei za vyakula na nchi zilizoathirika zaidi ni Nigeria, Ghana, Sierra Leone, na Mali.

Taarifa ya pamoja iliyotolewa na Shirika la Mpango wa Chakula duniani WFP, Shirika la kuhudumia watoto UNICEF na Ssirika la Chakula na Kilimo(FAO) imesema kuwa idadi ya watu waliokabiliwa na njaa wakati wa msimu wa mavuno imeongezeka mara nne katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Changamoto za kiuchumi ikiwa ni pamoja na mfumuko mkubwa wa bei na kudorora kwa uzalishaji wa ndani, vinatajwa kuchochea zaidi mgogoro huo wa njaa,Mashirika hayo yameonya kuwa watoto wapatao milioni 17 walio chini ya umri wa miaka mitano wana utapiamlo kutokana na uhaba wa chakula.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *