Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Mafuriko yaharibu nyumba 360, mashamba 1000 Urusi

Mamlaka katika mji wa Orenburg nchini Urusi imetoa wito kwa maelfu ya wakaazi kuhama mara moja kutokana na kuongezeka kwa mafuriko baada ya kingo za mito mikubwa kupasuka kufuatia theluji inayoyeyuka.


Naibu meya wa mji wa Orenburg Alexei Kudinov, alisema hapo awali kwamba zaidi ya nyumba 360 na karibu mashamba 1,000 yalikuwa yamefurika maji usiku kucha.


Kiwango cha maji kinaripotiwa kuongezeka kwa kasi katika eneo jingine la Urusi la Kurgan na katika nchi jirani ya Kazakhstan na hadi sasa watu takribani 100,000 wamehamishwa huku hali ya joto inayoongezeka ikizidi kuyeyusha theluji kubwa.


Kuongezeka kwa viwango vya maji pia kunatishia sehemu za kusini za Siberia Magharibi, bonde kubwa zaidi duniani la haidrokaboni na katika maeneo ya karibu na Mto mkubwa zaidi barani Ulaya wa Volga.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *