Akiongea mbele ya waandishi wa habari leo Machi 29, 2024, Kocha wa klabu ya Yanga, Miguel Gamondi amekiri kuwa atawakosa wachezaji wake watatu kesho kwenye mechi dhidi ya Mamelodi.
Wachezaji hao ni Khalid Aucho, Kouassi Attohoula Yao na Pacôme Zouzoua huku akiwa hana uhakika kama ataweza kuwatumia Aziz Ki na Djigui Diarra kwasababu bado hawajawasili nchini Tanzania wakitokea katika majukumu yao ya Timu ya Taifa.