Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

8 wakamatwa kwa kuvamia kumbi za starehe Shinyanga

Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limewaondoa hofu wakazi wa maeneo ya Ndala, Lubaga Majengo Mapya, na maeneo ya kati kati ya mji katika halmashauri ya manispaa ya Shinyanga, baada ya kuibuka kundi la vijana ambao wamekuwa wakivamia maeneo hayo hasa nyakati za usiku katika kumbi za starehe wakiwa na silaha za jadi kama vile mapanga na marungu kisha kufanya uhalifu kwa kuwaibia watu vitu mbali mbali zikiwemo fedha na simu za mkononi.

Akizungumzia tukio hilo kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga kamishna msaidizi wa polisi Kenedi Mgani amesema wanawashikilia vijana wanane kwa kuhusika na matukio hayo na kuongeza kuwa jeshi hilo linaendelea na uchunguzi ili kubaini mtandao zaidi unaohusika ,na upelelezi utakapokamilika vijana hao watafikishwa mahakamani.

Nao baadhi ya wakazi wa halimashauri ya manispaa ya Shinyanga wamelishukuru jeshi la polisi kwa kuwatia nguvuni vijana hao huku wakielekeza lawama zao kwa baadhi ya wazazi kutokuwa makini na uangalizi wa watoto hali inayopelekea kuingia katika makundi ya uahalifu na kulitaka jeshi hilo kuongeza nguvu zaidi katika baadhi ya maeneo ambako vitendo hivyo vimekuwa vikijitokeza mara kwa mara.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *