Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

76 Mbaroni kwa kumpiga Mkuu wa Kituo cha Polisi

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Kamishina Msaidizi wa Polisi, Shedrack Masija Amesema wanawashikilia watu 76 kwa tuhuma za kumpiga na kumjeruhi Mkuu wa Kituo cha Polisi Kabwe, kilichopo wilayani Nkasi na kuharibu mali mbalimbali za Serikali na watu binafsi.

Masija amesema tukio hilo limetokea Septemba 11, 2023 ambapo kundi la watu zaidi 20, walivamia Kituo cha Polisi na kumpiga mkuu wa kituo hicho na kuchoma moto uzio, kubomoa madirisha, kuharibu pikipiki mbili na kuharibu samani mbalimbali za kituo hicho.

Amesema chanzo cha kurugu hizo ilikuwa ni wananchi kumshinikiza mkuu wa kituo hicho awaachilie huru watuhumiwa wanane waliokuwa wamekamatwa na polisi, usiku wa Septemba 10, 2023 kwa kosa la kuchangisha fedha wananchi ili kuwaleta watu wanaodaiwa kujifanya waganga wa kienyeji (Lambalamba), wenye uwezo wa kuwabaini na kuwakamata wachawi.

Kamanda huyo amesema kuwa baada ya wananchi kuvamia kituo hicho na kubaini watuhumiwa hao hawapo kituoni hapo, walivamia baadhi ya maduka, nyumba za kulala wageni na kupora bidhaa mbalimbali kama vile magodoro, mafuta ya diezeli, petroli, mafuta ya taa, friji, magunia ya mpunga, simenti, Tv, makochi, mabati na bidhaa nyingine za madukani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *