Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

70% ya magonjwa ya binadamu yanatokana na wanyama

Wataalam wa Afya ya binadamu, Afya ya mifugo na jamii wametakiwa kushirikiana ili kupambana na asilimia 70 ya magonjwa ya binaadamu yatokanayo na wanyama.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amesema hayo wakati akifungua Kongamano la Tatu la Kisayansi la Mapambano ya Usugu wa Vimelea dhidi ya Dawa (UVIMADA) Jijini Arusha.

Waziri Ulega amesema matumizi yaliyokithiri ya dawa za Antibiotiki katika kukuza mifugo kwa kuchanganya na chakula cha mifugo kwa matumizi ya kila siku kwa wanyama wanapokuwa hawaumwi hupelekea magonjwa kwa mlaji wa mfugo huo.

Aidha, Waziri Ulega ametoa wito kwa wauzaji wa dawa na watengenezaji wa chakula katika kuchochea mapambano ya dawa dhidi ya vimelea sugu vya magonjwa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *