61 MBARONI KWA TUHUMA MBALIMBA MWANZA, DAWA ZA KULEVYA ZAHUSISHWA

Jeshi la polisi Mkoani Mwanza linawashikilia watuhumiwa 61 kwa tuhuma za kujihusisha na dawa za kulevya, kukiuka masharti ya leseni za biashara pamoja na matumizi ya dhana haramu za uvuvi katika wilaya za Ukerewe na Ilemela.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Naibu Kamisha wa Polisi, Wilbroad Mutafungwa amesema oparesheni hiyo ilianza Aprili 10, 2026 kufuatia taarifa za wananchi zilizotolewa katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya kagunguli Ukerewe.

Naibu Kamisha wa Polisi, Wilbroad Mutafungwa.

Kupitia oparesheni hiyo, watuhumiwa 16 wamekamatwa kwa matumizi na umiliki wa dawa za kulevya aina ya bangi wilayani Ukerewe huku watuhumiwa 3 walikamatwa na zana haramu za za uvuvi katika kata ya murutunguru.

Katika hatua nyingine polisi wamewakamata watuhumiwa kadhaa kwa kukiuka masharti ya leseni ya biashara katika baa na nyumba ya kulala wageni wilaya ya Ilemela makosa yanayochangia vitendo vya uhalifu.

Aidha kamanda Mutafungwa ameongeza kuwa oparesheni hiyo imefanyika kwa siku tatu mfululizo ambapo watuhumiwa 15 walikamatwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *