Rapa kutoka Marekani, 50 Cent, ameweka wazi kuipeleka ziara yake ya ‘The Final Lap Tour’, nchini Nigeria, huku tarehe bado haijatangazwa.
50 amesema hayo hivi karibuni kupitia ukurasa wake wa Instagram. Na kwa sasa msanii huyo yupo kwenye kusheherekea miaka 20 ya albamu yake ya Get Rich or Die Tryin.
Hii ni mara ya pili kwa staa huyo kutimba Nigeria ambapo mwaka 2004 alifika Afrika Kusini na Nigeria na alitumbuiza, 2008 alifika Angola, Tanzania na Afrika Kusini na 2012, alifika Somalia akiwa na World Food Program, kwaajili ya kutengeneza uwelewa wa chakula Bora.
