48 KUWANIA NAFASI MBALIMBALI ZA UONGOZI BAKWATA SINGIDA

Na Saulo Stephen – Singida. 

Jumla ya wagombea 48 wanatarajia kuwania nafasi mbalimbali za uongozi wa BAKWATA mkoa wa Singida katika uchaguzi mkuu wa chama hicho unaotarajiwa kufanyika siku ya Jumapili Octoba 12,2025.

Akizungumza na wanahabari ofisini kwake, Katibu wa BAKWATA mkoa wa Singida, Ustadh Omary Muna amesema uchaguzi huo utafanyika katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Singida kuanzia saa 4:00 asubuhi, ukihusisha wajumbe kutoka wilaya zote za mkoa wa Singida Viongozi watakaopatikana wataongoza shughuli za BAKWATA katika kipindi kijacho katika mkoa wa Singida.

Katibu wa BAKWATA mkoa wa Singida,Ustadh Omary Muna.

Aidha katibu huyo wa Bakwata mkoa wa Singida amesema maandalizi yote muhimu ya uchaguzi huo yamekamilika, huku akiwataka wagombea na wajumbe wote kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani, umoja, na kuzingatia misingi ya haki na maadili ya kidini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *