30 Wafukiwa na kifusi, wawil wafariki

Watu wawili wamefariki dunia baada ya kuangukiwa na kifusi cha mchanga wakati wakichimba dhahabu katika Mgodi wa Kanegere wilaya ya Mbogwe Mkoani Geita.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Geita Kamishina msaidizi wa polisi Safia Jongo amesema tukio hilo limetokea Septemba 10, 2023 ambapo watu 30 walifukiwa na kifusi wakati wakichimba dhahabu na 28 walifanikiwa kuokolewa wakiwa hai huku wawili wakipoteza maisha.

Kamanda Jongo amesema wachimbaji hao maarufu kama Manyani walivamia katika mgodi huo ambao ulikuwa umefungwa kufanya shughuli za uchimbaji hivyo walipita njia za panya na kuanza kuchimba na kuwataka wachimbaji wadogo kufuata maelekezo yanayotolewa na serikali.

Baadhi ya manusura wa ajali hiyo akiwemo wamesema waliingia ndani ya shimo hilo majira ya saa tano usiku na kuwakuta wenzao zaidi ya 20 wakichimba dhahabu na baada ya kuwaomba nao wachimbe wenzao waliwakatalia kisha wakatoka nje ya shimo na baadae waliporudi walikuta wenzao wamedondokewa na kifusi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *