Na Saulo Stephen – Singida.
Chama cha Napinduzi (CCM), kimepanga kumaliza changamoto ya maji kwa kutekeleza Mradi mkubwa wa maji utakaohudumia wananchi wa wilaya ya Ikungi mkoani Singida, pindi chama hicho kitakapofanikiwa kupata ridhaa ya kushika dola katika uchaguzi mkuu wa Octoba 29 mwaka huu.
Hayo yamebainishwa na Mgombea mwenza wa kiti cha urais wa CCM, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi wakati akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Ikungi, kwenye mkutano wa kampeni za chama hicho, uliofanyika eneo la Puma jimbo la Ikungi Magharibi Mkoani Singida.

Amesema kutokana na upatikanaji wa huduma ya maji kuwa asilimia 73 kwa sasa katika wilaya ya Ikungi, Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ambae pia ni Mgombea wa nafasi hiyo katika uchaguzi wa mwaka huu imepanga kuongeza upatikanaji wa maji kupitia mradi huo utakaofanya upatikanaji wa maji kufikia asilimia 85 katika wilaya ya Ikungi.
Katika hatua nyingine Dkt.Nchimbi amewaomba wanaikungi ifikapo Octoba 29 mwaka huu 2025 wawachague madiwani wanaotokana na chama cha mapinduzi, vilevile wabunge watokanao na chama hicho ambao ni Chief Mgonto kutoka jimbo la Ikungi Mashariki pamoja na Elibariki Kingu kutoka jimbo la Ikungi Magharibi kadhalika Mgombea wa Urais kupitia CCM ambae ni Dkt.Samia Suluhu Hassan.



