Ikiwa ni takribani siku chache za minong’ono hatimaye Simba SC imetangaza kuachana na Kocha wake, Fadlu Davids kwa makubaliano ya pande mbili.
Tayari Kocha huyo raia wa Afrika Kusini anayehusishwa kujiunga na klabu ya Raja Casablanca ameushukuru Uongozi, wachezaji, benchi la ufundi na mashabiki wa Simba SC kwa mshikamano.


