256 WAPIMA VVU MKESHA WA MWENGE MSALALA, MMOJA AKUTWA NA MAAMBUKIZI

Jumla ya wanachi 256 katika Halmashauri ya Msalala wamepata huduma ya kupima  maambukizi ya virusi vya ukimwi kwenye mkesha wa mwenge wa uhuru kati yao wanaume wakiwa 134 na wanawake wakiwa ni 122 huku mwanamme mmoja akikutwa na ugonjwa huo huku kukiwa hakuna mwaanchi aliyekutwa na ugojwa wa maralia,

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Frank Nkinda wakati akisoma taarifa ya mkesha wa mwenge wa Uhuru  mbele ya Kiongozi wa Mbio za mwenge kitaifa Ismail Ussi.

Amesema, “katika mkesha wa mbio za mwenge jumla ya wananchi 256 wamepata huduma ya kupima maambukizi ya virusi vya ukimwi na manaume mmoja amekutwa na maambukizi huku wananchi waliopima ugonjwa wa maralia hakuna aliyekutwa na ugonjwa huo.”

Nkinda ameongeza kuwa, mkesha wa mwenge umefanikiwa kukusanya uniti 16 za damu na Pamoja mradi wa mradi wa nishati safi wa majiko manifu.

“Kiongozi wa mbio za mwenge tunapenda kukujulisha kuwa katika mkesha wa Mwenge uniti 16 za damu zimekusanywa na mradi wa utunzaji mazingira tuna majiko sanifu Matano yenye thamani ya shilingi milioni mbili kila moja,” ameongeza Nkinda.

Kwa upande wake kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru 2025 Ismail Ali Ussi amewataka viongozi wa halmashauri ya msalala kusimamia kauli mbiu ya mwenge kwa kuhamasisha wananchi kujitokeza kupiga kura kwa utulivu na amani.

“Niwaombe sana ndugu zangu kama ujumbe wa mbio za mwenge unavyosema,nendeni mkahakikishe mnahamasisha wananchi wanajitokeza kushiriki uchaguzi mkuu kwa amani na utulivu,” amesema Ussi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *