Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

2025 CCM inapata ushindi

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda, leo amepokelewa rasmi katika ofisi ndogo za chama hicho, Lumumba jijini Dar es Salaam baada ya kuteuliwa siku kadhaa zilizopita.

Akizungumza katika hafla hiyo, Makonda amesema ni mapema sana kwa yeye kuanza kuzungumza kwa sababu bado yapo mambo mengi anayopaswa kujifunza.

Makonda Amesema atashirikiana na viongozi na wanachama wote, kuhakikisha CCM inapata ushindi siyo kwenye chaguzi za 2024 na 2025 pekee, bali katika chaguzi zote zitakazokuja.

Kwa upande wake Aliyekuwa Katibu Mkuu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Sophia Mjema katika hotuba yake ya kumkaribisha, Makonda,amemtaka kuhakikisha chama hicho kinapata ushindi katika uchaguzi ujao wa serikali za mtaa 2024 na Uchaguzi Mkuu wa 2025.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *