Watu 13 wameripotiwa kufariki dunia, huku wengine 32 wakijeruhiwa katika ajali ya basi iliyohusisha basi la abiria la kampuni ya Allys Star lenye namba za usajili T 178 DVD, baada ya basi hilo kugonga kichwa cha treni, katika eneo Manyoni, mkoani Singida.
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Dk.Furaha Mwakafwila amesema Hospitali ya Wilaya ya Manyoni ilipokea miili ya watu 9 waliofariki papo hapo baada ya ajali kutokea.
Amesema wengine wanne ambao ni kati ya majeruhi 32 waliopelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Manyoni na Hospitali ya St Gasper iliyopo Halmashauri ya Itigi walifariki wakati wakipatiwa matibabu katika hospitali hizo.
Mkuu wa Mkoa Singida,Peter Serukamba na Kamanda wa Polisi wa Singida, ACP Stellah Mutahibirwa na maafisa wengine wa vyombo vya ulinzi na usalama mkoa wa Singida wapo eneo la tukio.