Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Rais Samia Aagiza Uchunguzi,Kupatiwa Taarifa ya Kifo Cha Kiongozi wa CHADEMA

Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amegiza Vyombo vya Uchunguzi kumpatia taarifa ya kina haraka kuhusu tukio baya la mauaji ya Kiongozi wa CHADEMA Ali Kibao na mengine ya namna hiyo.

“Kwa masikitiko makubwa nimepokea taarifa ya mauaji ya kiongozi wa CHADEMA Bwana Mohamed Ali Kibao. Natoa pole kwa viongozi wa chama hicho, familia ya Mzee Kibao, ndugu, jamaa na marafiki.

Nimeagiza vyombo vya uchunguzi kuniletea taarifa ya kina kuhusu tukio hili baya kabisa na mengine ya namna hii haraka. Nchi yetu ni ya kidemokrasia na kila raia ana Haki ya kuishi. Serikali ninayoiongoza haivumilii vitendo vya kikatili vya namna hii”ameandika Rais Dkt.Samia

Septemba 8,2024, ilielezwa kwamba Mwili wa aliyekuwa Mjumbe wa Sekretarieti ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA)Taifa na Msaidizi wa Katibu Mkuu umekutwa hospitali ya Mkoa wa Kinondoni, Mwananyamala katika chumba cha kuhifadhia maiti ukiwa umeharibika.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo kupitia ukurasa wa mtandao wa X(zamani Twitter) na Boniface Jacob(Boniyai) ilisema “mwili wa Ali Mohammed Kibao ulikutwa umetupwa jana(Septemba 7,2024) alfajiri maeneo ya Ununio(jirani na viwanja vya NSSF) ukiwa na majereha makubwa sehemu za usoni kiasi ndugu zake kupata tabu kuutambua kirahisi”

Jacob alieleza kuwa “kwa mujibu wa wenyeji wa Ununio ambao ni walima mchicha,wanasema Jana asubuhi walitoa taarifa kwa Jeshi la Polisi baada ya kuona mwili wa mtu mzima, mweupe mwenye asili ya kiarabu ambaye baadae jana jioni ndugu waliutambua kuwa ni mwili Ali Mohammed Kibao ukiwa na majeraha”

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ni kuwa Kibao kuna namba ya simu ilikuwa ikiwasiliana naye mara kadhaa nyuma kabla ya yeye kutekwa Ijumaa ya Septemba,06,2024.

Jana Septemba 7,2024 Katibu Mkuu wa Chadema John Mnyika alizungumza na waandishi wa habari na kueleza kuwa Kibao alitekwa eneo la Kibo Complex Tegeta Dar Es Salaam na watu wenye silaha ikiwemo bunduki kisha wakaondoka naye.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *