VIDEO: 12% tu wanafunzi wameripoti kuanza masomo 2024

Maandalizi hafifu ya wazazi na walezi mkoani Geita imetajwa kuwa sababu kubwa ya wanafunzi wa darasa la awali, darasa la kwanza pamoja na kidato cha kwanza kuchelewa kuanza masomo kwa muhula mpya wa masomo 2024.

Akizungumza na Jambo FM, Afisa Elimu Mkoa wa Geita mwalimu Antony Mtweve amesema licha ya serikali kujenga miundombinu bora kwa shule za msingi na sekondari pamoja na kuondoa ada kwa wanafunzi bado kuna changamoto kubwa ya wanafunzi kuripoti ambapo hadi Januari 11, 2024 asilimia 12 tu ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza ndiyo wameaanza masomo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *